Mabingwa wa nchi Simba wako katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo ligi itakaporejea
Vinara hao wa ligi wamejikusanyia alama 71 baada ya kushuka dimbani mara 28, kimahesabu, wanatakiwa kushinda mechi tano tu kati ya 10 zilizosalia ili kutawazwa kuwa mabingwa kwa mara nyingine
Katika mechi zilizosalia, Simba itacheza mechi nne jijini Dar es salaam na mechi sita mikoani
Mechi zilizobaki ambazo zitapigwa jijini Dar es salaam ni dhidi ya Alliance Fc, Mbao Fc, Ruvu Shooting na Mwadui Fc
Mechi zita zilizobaki mikoani ni dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Namungo Fc, Ndanda Fc, Prisons Fc na Mbeya City
Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amebainisha kuwa ligi huenda ikarejea karibuni lakini pia pengine kutakuwa na utaratibu tofauti kwa mechi hizo kupigwa kwenye viwanja vichache ambavyo vitapendekezwa badala ya timu kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine