Simba na rekodi za kibabe katika historia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 May 2020
Simba na rekodi za kibabe katika historia

Mwaka 1977, Simba iliweka rekodi katika mechi za watani wa jadi kwa kuifunga Yanga mabao 6-0. Zaidi ya miaka 42 rekodi hiyo haijafikiwa.

Mwaka 1938, Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikuwa timu ya kwanza kucheza na jezi ilipocheza na timu ya kombaini ya mabaharia wa meli zinazotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Mwaka 1941, (Sunderland) kwa sasa Simba SC ilikuwa timu ya kwanza nchini kuvaa viatu kwenye mechi rasmi ya mashindano dhidi ya timu ya jeshi la maji la mkoloni la Afrika Mashariki.

Mwaka 1959, kabla ya uhuru wa Tanganyika, kipindi hicho ikiitwa Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikwenda Ethiopia na ikawa timu ya kwanza kutoka nchini kupanda ndege. Ilikwenda kwa mwaliko wa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia.

Mwaka 1965, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania.

Mwaka 1968, Simba ilikuwa timu ya kwanza nchini kumiliki basi lake.

Mwaka 1974, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kuwa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati. Pia mwaka huo Simba ikawa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika.

Mwaka 1979, Simba ilikuwa klabu ya kwanza na ya pekee duniani kwenye mashindano ya mabara tofauti kufungwa nyumbani magoli 4-0 na kushinda ugenini magoli 5-0 (dhidi ya Mufulira Wanderers).

Mwaka 1993, Simba ilikuwa klabu pekee nchini kuwahi kufika fainali ya mashindano yanayoandaliwa na CAF (kwa sasa Kombe la Shirikisho) na kucheza fainali na klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Simba ndio mabingwa wa muda wote wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati (makombe 6).

Mwaka 2003, Simba ilivunja rekodi ya Zamalek ya Misri kwa kuitoa kwenye Ligi Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya makundi. Zamalek walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Simba ndio klabu yenye makombe mengi ya jumla kuliko klabu yoyote Afrika Mashariki, ikiwa na vikombe rasmi vya kimashindano 58. Hakuna klabu yoyote zaidi yetu yenye mataji rasmi 58 kwenye nchi za Afrika Mashariki.

Kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Simba ndio klabu pekee ambayo kurasa zake zote za mitandao ya kijamii zimethibitishwa (verified), pia ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafuasi (followers) 2.2M

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
6h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
9h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’