Mshambuliaji wa Simba Miraji Athumani amesema yuko tayari kurejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu
Miraji maarufu kama Sheva mwaka huu hajaonekana kabisa uwanjani kutokana na majeraha aliyopata mwaka uliopita
Mwezi uliopita Sheva alianza mazoezi mepesi kabla ya madaktari kumthibitishia kuwa amepona
"Kwa sasa nimepona majeraha yaliyokuwa yakinisumbua niko tayari kuitumikia timu yangu pale kocha atakaponihitaji," amesema
"Nimekaa nje kwa muda mrefu, nilikuwa nikiumia sana kwa kuwa sikuweza kuisaidia timu yangu lakini sasa nafurahi ligi itakaporejea naweza kuwa na mchango," aliongeza Sheva
Kwenye mechi 10 za kwanza msimu huu, Sheva aliifungia Simba mabao sita huku akitengeneza mabao mawili
Hata hivyo majeraha ya kifundo cha mguu yalimfanya akae nje kwa zaidi ya miezi minne