Uongozi wa klabu ya Simba umeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha ASP Masoud Mohamed ambaye alifikwa na umauti jana huko Ukerewe, Mwanza
Simba imemtaja ASP Masoud alikuwa mdau mkubwa wa mabingwa hao wa nchi
"Shabiki wetu mwandamizi ASP Masoud Mohamed amefariki leo (jana) huko Ukerewe. Tunatoa pole kwa familia yake na tunawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu, lakini pia tunatoa pole kwa Jeshi la Polisi na wote walioguswa na msiba huu. Poleni Wanasimba," ilisema taarifa ya Simba


Kifo cha Afande Masudi kimegusa watu wengi kutokana na jinsi alivyoishi vyema na kusaidia watu
Afande Masudi pia alikuwa kiongozi na mfano katika kutoa elimu na mafunzo ya dini ya kiislamu
Mwenye ez Mungu ailaze roho yake mahali pema, peponi Amen..