Kagere apiga hesabu za kurejea nchini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 May 2020
Kagere apiga hesabu za kurejea nchini

Baada ya Rais John Magufuli kutangaza kuwa anafikiria kurejesha mikiki mikiki ya ligi kuu, mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere anafikiria utaratibu utakaomuwezesha kurejea nchini mapema

Kagere ambaye ni raia wa Rwanda, anakabiliwa na changamoto ya usafiri baada ya Rais wa nchi hiyo Paul Kagame, kufunga mipaka kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19.

Rafiki wa karibu wa mshambuliaji huyo, amesema Kagere tangu aliposikia kauli ya Rais Magufuli, kila mara anaulizia kinachoendelea Tanzania.

Rafiki huyo wa Kagere alisema siku ya kwanza tu, Rais Magufuli alipoongea alimtaka amfafanulie kila kitu kama ametaja tarehe ya ligi hiyo kurejea.

"Kagere huko aliko hatulii, kila mara anaulizia maendeleo ya Ligi kurudi, siku ile tu kasikia Rais kaongea, aliniambia nimuelezee kwa undani nini amekisema," amesema

Kagere ndiye kinara wa mabao ligi kuu ya Vodacom akiwa amefunga mabao 19, mabao nane zaidi ya Yusufu Mhilu na Reliants Lusajo wanaomfuatia

Mbabe huyo wa kuzifumania nyavu, anataka kuvunja rekodi ya mabao 23 aliyojiwekea msimu uliopita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
35m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’