Ajibu awapa ujumbe wanaosema ni mvivu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 May 2020
Ajibu awapa ujumbe wanaosema ni mvivu

Kiungo fundi wa Simba Ibrahim Ajibu maarufu kama 'cadabra' au mzee wa 'makorokoro' amesema suala la kuambiwa ni mvivu halimsumbui kwani halikuanza leo

Ajibu amefichua kuwa hata wakati anaishi nyumbani kwao alikuwa akikumbana na changamoto hiyo

"Ngoja nikwambie ishu ya watu kusema mimi ni mvivu haikuanza leo na wala hainiumizi kichwa"

"Tangu naishi kwetu nimekuwa nikiambiwa kwamba mimi mvivu lakini ninajua ninachokifanya na shabaha yangu ilipo.

"Sikasiriki kuitwa mvivu, nafanya mazoezi yangu na ninafanya kile ninachoambiwa na makocha

"Leo hii naishi kwangu na bado ninaambiwa ni mvivu. Hivyo ni maneno tu ambayo hayaniumizi kichwa kwa sababu najua kile ninachofanya na mafanikio nayaona" aliongeza Ajibu

Juzi katika mahojiano yake na Mwanahabari ShaffihDauda, Ajibu alibainisha uamuzi wake wa kurejea Simba licha ya TP Mazembe kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili

"Nilichagua kucheza Simba kwa sababu walinipa ofa nzuri zaidi kuliko Mazembe na Yanga. Lakini pia niliondoka Simba nikiwa bado mdogo, sasa nimepevuka na ulikuwa ni wakati mwafaka kwangu kurejea"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’