Changamoto hizi zinaweza kujitokeza ligi itakaporejea

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 May 2020
Changamoto hizi zinaweza kujitokeza ligi itakaporejea

Wakati  Ligi Kuu Tanzania Bara ikitarajiwa kuanza hivi karibuni wadau wa soka wanasema hawategemei kuona ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji kutokana na sababu mbalimbali.

Baadhi ya wadau wametoa maoni yao wakisema  kuna timu zitakazopambana kukwepa kushuka daraja, kuna wachezaji wanawaza kumaliza mikataba na wengine kutawaliwa na uvivu baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu bila mazoezi ya pamoja.

Mchambuzi Dominic Salamba alisema baadhi ya wachezaji hawatachukulia kwa uzito Ligi itakapoanza kwa kuogopa kuumia kutokana na msimu kuelekea mwishoni na wako waliotakiwa na timu nyingine hawataonyesha kiwango bora wakijua wazi wapo kwa ajili ya kukamilisha ratiba.

"Hatutategemei kiwango kikubwa kwa sababu wanajua wanacheza kwa muda mfupi kuna suala la mikataba, wengine wanaweza kuogopa kuumia na kuna ambao uzito utakuwa umeongezeka kwa kuwa wamekaa nyumbani muda hivyo ushindani utakuwa wa kawaida, " Salamba alinukuliwa na HabariLeo

Kuhusu ushindani katika timu alisema utahamia zaidi kwa timu zilizoko katika hatari ya kushuka daraja na zile zinazogombania nafasi ya pili ambazo ni Azam FC na Yanga zilizotofautiana kwa pointi tatu.

Naye mchambuzi na mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Mayai alisema anategemea kuona kiwango cha ligi kikiporomoka siyo tu kwa Tanzania bali hata zile za Ulaya na kutoa sababu wachezaji hawajakaa katika mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu.

Alisema licha ya makocha wengi kutoa programu za mchezaji mmoja mmoja wakati wakiwa nyumbani haitoshi kurejesha kiwango kwa vile hufanya bila usimamizi akichoka hupumzika tofauti anapokuwa katika mazoezi ya pamoja.

Kuhusu timu, Mayay hakutofautiana na Salamba kwani alizitaja Yanga na Azam kushindana na kwenye timu zitakazoshuka akiitaja Singida kuwa imekata tamaa .

Naye Kocha wa zamani wa Kagera Sugar na KMC, Mrage Kabange alisema hategemei kuona ushindani kwa sababu yupo anayejulikana kuwa ni bingwa ambaye ni Simba aliyewaacha wengine mbali kwa tofauti ya zaidi ya pointi 20

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’