Simba kumpotezea rasta wa Asante Kotoko

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 May 2020
Simba kumpotezea rasta wa Asante Kotoko

Yule mshambuliaji rasta aliyekuwa akicheza klabu ya Asante Kotoko ya Ghana, Yacouba Sogne ni miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa kuwaniwa na mabingwa wa nchi, Simba

Katika ripoti ya kocha Sven Vandenbroeck, inaelezwa Mbelgiji huyo ametaka kuongezewa mshambuliaji mmoja ambaye atashirikiana na Meddie Kagere na John Bocco ambao bado wanaendelea kudunda Msimbazi kwa kuwa wana mikataba ya muda mrefu

Kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Simba imepokea taarifa za Yacouba kupitia wanaojitambulisha kuwa Mawakala wake ambao wametuma taarifa zao kwa Mtendaji Mkuu wa mabingwa hao wa nchi Senzo Mazingisa

Senzo ameeleza kuingiwa na wasiwasi kutokana na msululu wa taarifa anazotumiwa kutoka kwa Mawakala hao hivyo upo uwezekano mkubwa watampotezea

Pamoja na kuhusishwa na Yacouba ambaye amemaliza mkataba kunako klabu ya Asante Kotoko, mabingwa hao wa nchi pia wanatajwa kumuwania mshambuliaji wa Orlando Pirates, Mzambia Justine Shonga

Inaelezwa uwepo wa Senzo, unaweza kurahisisha upatikanaji wa mshambuliaji huyo licha ya kudaiwa kuwa thamani yake ni zaidi ya Tsh Bilioni 1.6

Mwezi Januari Senzo aliiwezesha Simba kumnasa winga Luis Miquissone kutoka klabu ya Mamelodi Sundons ambaye alikuwa akicheza kwa mkopo UD Songo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
28m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’