Dilunga afurahi kutambuliwa na nyota Everton

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 May 2020
Dilunga afurahi kutambuliwa na nyota Everton

Unakumbuka staili ya ushangiliaji ambayo aliitumia kiungo mshambuliaji wa Simba Hassan Dilunga baada ya kuwatungua waajiri wake wa zamani Mtibwa Sugar mchezo wa ligi kuu uliopigwa Februari 11 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri na Simba kuondoka na ushindi wa mabao 3-0?

Baada ya kufunga moja ya mabao kwenye mchezo huo, Dilunga alikwenda kwenye kibendera cha kona na kuonyesha ishara ya kupigana na kibendera hicho na baadae kuwaomba radhi mashabiki wa Mtibwa ambao bado wanamkumbuka

Sasa nyota wa zamani wa Everton Tim Cahil kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter alibandika video ya tukio hilo ambayo imepata umaarufu sana duniani

Dilunga amelizungumzia tukio hilo kama faraja kubwa kwake hasa ikizingatiwa heshima aliyonayo Cahil kwenye ulimwengu wa soka

"Kwa kweli nimejisikia furaha sana kwa Cahil kutumia muda wake kuposti video ile kwenye ukurasa wake. Nilipofanya jambo lile sikuwa na fikra kuwa siku moja litakuwa kubwa na kuonekana dunia nzima, nafurahi kwa utambuzi huo niliopewa"

Enzi zake Cahil naye alikuwa akitumia mtindo huo wa kushangilia kwa kupigana na kibendera cha kona pale alipofunga bao

Dilunga ameahidi kuendelea na mtindo huo wa ushangiliaji kila atakapofunga wakati mwingine

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
17h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’