Mshambuliaji wa Orlando Pirates Justine Shonga ameingia tena kwenye rada za klabu ya Simba ambapo safari hii mabingwa hao wa nchi wamepania kumbeba 'mazima'
Msimu uliopita Simba ilijaribu kumsajili Shonga hata hivyo iliachana nae baada ya Orlando Pirates kutaka dau la usajili ambalo lilikuwa zaidi ya Tsh Bilioni moja
Inaelezwa Pirates wamepunguza dau na wako tayari kumuachia kwa timu ambao itatoa angalau dola laki tatu na nusu (Tsh Milioni 800)
Mpango wa Simba kumrudia Shonga umefichuliwa na Mwandishi mmoja wa Habari huo Ghana aliyefahamika kwa jina la Nuhu Adams
Tangu atue kunako klabu hiyo Shonga raia wa Zambia amekuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza jambo linalomfanya ashinikize kuondoka
Msimu uliopita Zamalek pia ilikuwa tayari kumsajili lakini kikwazo kikawa katika dau la usajili wanalotaka Pirates (Bili 1.3)
Lakini mchezaji huyo ni miongoni mwa nyota wanaopokea mshahara mkubwa kwenye kikosi cha Pirates akivuta mkwanja unaofikia Tsh Milioni 38 kwa mwezi