May 06 2012 itaendelea kubaki kwenye kumbukumbu za wadau wa soka nchini ikiwa siku ambao mabingwa wa nchi Simba waliwafumua watani zao Yanga kwa kuwabugiza mabao 5-0
Hiyo ilikuwa mara ya pili Simba inapata ushindi mkubwa zaidi dhidi ya watani zao hao kwani mwaka 1976 kipigo cha mabao 6-0 kiliwahusu wanajangwani hao
Siku hiyo Simba ilikuwa bora kwelikweli, ilitawala mchezo kila idara tena ikifanya hivyo huku ikiwa tayari imejihakikishia ubingwa
Simba ilifunga mabao yake kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyefunga mabao mawili huku mabao mengine yakifungwa na Felix Sunzu, Juma Kaseja na marehemu Patrick Mafisango
Tujikumbushe matukio mbalimbali yaliyojiri kwenye mchezo huo;








ADVERTISE HERE