Simba yasubiri kauli ya TFF kurejea mazoezini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 May 2020
Simba yasubiri kauli ya TFF kurejea mazoezini

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazngisa amesema tamko la Rais wa Tanzania Dk John Magufuli limewapa faraja kuwa ligi itarejea na kuwa na uhakika wa kutetea ubingwa wao kwa kucheza mechi zilizobaki

Senzo amesema klabu ya Simba imejipanga kuendeleza pale walipoishia kwa kuwa hesabu zao ni kuchukua ubingwa kwa kumalizia mechi zilizobaki kwa kishindo

Amesema wanasubiri maelekezo ya TFF ili wawarejeshe wachezaji wao kwa ajili ya mazoezi

"Tumeipokea kwa furaha kauli ya Rais Magufuli, imetupa faraja sasa tunaweza kurejea kwenye soka muda siyo mrefu. Lakini bado tunaendelea kusubiri TFF na Bodi ya Ligi itoe tamko kabla hatujatoa tamko lolote la kuanza kwa programu zetu, " amesema Senzo.

Wakati ligi ikiwa imesimama kwa zaidi ya siku 49, benchi la ufundi la klabu ya Simba liliwapa wachezaji program maalum ya mazoezi ambayo wanafanya huko majumbani kwao

Kocha Sven vandenbroeck amesema wamekuwa wakifuatilia program hizo ambapo pia amesema wachezaji wote watakaporejea watajiridhisha kama walikuwa wakifuata maelekezo waliyowapa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’