Ajubu ataja sababu ya kuitosa TP Mazembe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 May 2020
Ajubu ataja sababu ya kuitosa TP Mazembe

Kiungo fundi wa mpira Ibrahim Ajibu Migomba kwa mara ya kwanza amezungumzia uamuzi wake wa kujiunga na klabu ya Simba licha ya vigogo wa soka barani Afrika TP Mazembe kuitaka saini yake usajili wa mwaka jana

Ajibu amesema aliamua kuipotezea ofa hiyo baada ya kupokea ushauri kutoka kwa familia yake na wadau mbalimbali wa soka nchini akiwemo nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye aliwahi kucheza TP Mazembe

"Nilifikia uamuzi wa kusaini Simba baada ya kujadiliana na familia yangu na wadau. Lakini pia ofa ya Simba ilikuwa nono kuliko ofa ambayo waliitoa Mazembe," alisema Ajibu

"Niliongea na Samatta (Mbwana) ili anipe uzoefu wake kuhusu klabu ya TP Mazembe. Akanifahamisha mengi lakini mwisho wa siku akaniambia uamuzi wa mwisho nifanye mwenyewe kwani hataki kuingia kwenye lawama pale mambo yatakapokwenda kinyume"

"Alinishauri niende nikacheze mpira sehemu ambayo nitakuwa na furaha. Lakini kubwa zaidi mimi kama mchezaji naangalia maslahi yangu. Kuna maisha baada ya mpira, sitaki nije kuonyeshewa vidole kuwa sikufanya jambo la maana pamoja na kuwa na kipindi kizuri wakati nacheza soka," alisema

Inaelezwa klabu ya TP Mazembe ilimpa Ajibu ofa inayofikia Tsh Milioni 60 wakati klabu ya Simba ilimchukua kwa dau la Tsh Milioni 80

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’