Waziri ataka vilabu visaidiwe kiuchumi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 May 2020
Waziri ataka vilabu visaidiwe kiuchumi

Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema wanaendelea kujadiliana na vyombo vinavyosimamia michezo nchini kuangalia jinsi watakavyoweza kurejesha michezo baada ya tamko la Rais Dk John Magufuli

Akizungumza baada ya kikao alichofanya na wadau hao jana, Dk Mwakyembe alisema ameliagiza Baraza la Michezo na Taifa (BMT) na TFF kuangalia jinsi wanavyoweza kuvisaidia vilabu kiuchumi ili kuweza kumudu gharama pale ligi itakaporejea

"Tumewaagiza BMT na TFF wawasiliane na FIFA, CAF ili kuomba fedha za kusaidia vilabu wakati huu wa changamoto ya corona"

"Ligi itakaporejea, kwa mechi kuchezwa bila ya mashabiki, timu zitakuwa kwenye wakati mgumu sana"

"Huu ni wakati ambao vilabu vinapaswa kusaidiwa na vyombo hivi ambavyo tunafahamu vina pesa ya kutosha," amesema Dk Mwakyembe

Tayari FIFA imetangaza kutoa mgawo wa zaidi ya Dola Milioni 150 kwa Wanachama wake katika jitihada za kuwasaidia kutimiza majukumu yao wakati huu wa kukabiliana na corona

TFF inatarajiwa kupokea zaidi Tsh Bilioni moja kutoka mgawo huo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’