Kiungo mkabaji wa Simba Jonas Mkude ni miongoni mwa wachezaji bora sana kwa sasa hapa Tanzania pengine na ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na umahiri wake
Jana ziliibuka tetesi kuwa magwiji wa soka barani Afrika vilabu vya Mamelodi Sundowns, TP Mazembe na Al Ahly zinatajwa kuwania sahihi ya mwamba huyo ambaye amedumu Msimbazi kwa misimu 10
Inaelezwa TP Mazembe ilijaribu kumsajili msimu uliopita hata hivyo mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' aliwazidi ujanja na kumuongezea mkataba wa miaka miwili
Hivyo kwa sasa Simba haina wasiwasi wa kumpoteza kwani kama ikitokea wataletewa ofa mezani, utakuwa 'mpunga' wa maana ambao utawawezesha kuziba nafasi yake
Mkude anatajwa kuwa miongoni mwa viungo wenye uwezo wa kupiga pasi kwa umahiri mkubwa