Mohammed Rashid afunguka kilichomkwamisha Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 May 2020
Mohammed Rashid afunguka kilichomkwamisha Simba

Mshambuliaji wa zamani wa Simba Mohammed Rashid ambaye kwa sasa anaichezea Polisi Tanzania, amesema kitendo cha mashabiki kuhitaji matokeo ni moja ya mambo yaliyosababisha kutopata namba ya kudumu katika kikosi cha Simba.

Rashid ambaye amewahi kucheza Simba kabla ya kwenda Polisi Tanzania alisema mashabiki wa timu kubwa hawana subira wanaamini kila mchezaji anayesajiliwa anatakiwa kufanya vizuri kila anapopata nafasi ya kucheza.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rashid alibainisha licha ya changamoto za kupata upinzani wa namba kutoka kwa wachezaji wazoefu kama John Bocco lakini anaamini presha ni sababu iliyomfanya kushindwa kuonesha uwezo wake.

"Unaweza ukafanya vizuri kwenye timu zingine lakini ukifika timu kubwa mashabiki hawana subira wanataka ukipewa nafasi uoneshe kitu, ukikosea basi wanakosa imani na wewe ndicho kilichonitibulia mimi," Rashid alinukuliwa na HabariLeo

Rashid anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alisajiliwa na Simba akitokea Klabu ya Tanzania Prison baada ya kuonesha uhodari wa kufumania nyavu kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Rashid alisema wakati anajiunga Simba alikutana na wachezaji watano wote wakicheza nafasi za mbele akiwemo Bocco, Meddie Kagere, Marcelo Kaheza, Clatous Chama na Juma Rashid hivyo mchezaji aliyekuwa anafanya vizuri alikuwa anapata namba ya kudumu kikosi cha kwanza.

“Ili kuwa kikosi cha wachezaji kinachomaliza mchezo kwa ushindi kinakuwa na nafasi kubwa ya kucheza mchezo unaokuja kwa kuwa kinakuwa na morali ya ushindi,” alisema Rashid

Kabla ya kutua Polisi Tanzania, Mo Rashid aliitumikia KMC kwa mkopo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
20h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’