Kiungo fundi wa Simba Ibrahim Ajibu amepata ofa huko Afrika Kusini kwenye moja ya timu inayoshiriki ligi kuu, imefahamika
Nyota huyo aliyetua Simba msimu huu akitokea klabu ya Yanga, alipaswa kwenda kufanya majaribio lakini changamoto ya corona imepelekea mpango huo kusitishwa kwa muda
Mmoja wa viongozi waandamizi wa klabu ya Simba ameeleza kuwa klabu hiyo haitamzuia Ajibu kwenda nje kama dili lake litafanikiwa
"Siku zote Simba tumekuwa tukiweka mbele maslahi ya wachezaji wetu, Kwani kufanikiwa kwa Ajibu kutafungua milango kwa wachezaji wengine"
Msimu huu haukuwa mzuri sana kwa Ajibu ndani ya kikosi cha Simba kutokana na ushindani mkubwa wa namba katika nafasi anayocheza
Hata hivyo amekuwa akifanya vizuri kila anapopewa nafasi na kocha Sven Vandenbroeck