Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema wamepokea kwa furaha kauli ya Rais Dk John Magufuli ambaye amesema siku za mbele anafikiri kuruhusu ligi iendelee kuchezwa
Manara amesema uamuzi wa kuruhusu ligi ichezwe bila ya mashabiki ni sahihi na sasa utaondoa utata, bingwa atapatikana uwanjani
"Tunamshukuru sana Rais sasa ligi inaweza kuchezwa bila watazamaji na bingwa halali kupatikana na ikiwapendeza inaweza kuchezwa katika kituo kimoja. Timu zote zikaja Dar, kama itakuwa ni ngumu kusafiri kila siku"
"Kwa mara nyingine Rais wangu unaonyesha uongozi ni nini. Haya wazee wa mbeleko njooni uwanjani sasa, akisema Rais ni amri sio ombi," ameandika Manara kweye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
ADVERTISE HERE