Rais Magufuli amaliza utata VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 May 2020
Rais Magufuli amaliza utata VPL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amesema siku za mbele ataruhusu ligi ziendelee nchini hata ikiwezekana bila ya mashabiki ili kuwapa fursa wanamichezo kuendelea kutimiza majukumu yao

Akizungumza mapema leo Mjini Chato katika hafla ya kumuapisha Waziri wa Katiba na Sheria Dk Mwigulu Nchemba ambaye aliteuliwa jana kuchukua nafasi ya marehemu Dk Augustine Mahiga,Β  Rais Magufuli amesema takwimu za maambukizi ya corona zinaonyesha kwa wanamichezo na watu wanaofanya mazoezi mara kwa mara hawapati maradhi hayo kwa urahisi

"Siku zinazokuja mbeleni, ninafikiria kuruhusu hata ligi iendelee ili watu wawe wanacheza na wanaangalia kwenye TV na kadhalika, tutaweka utaratibu mzuri tu baada ya kushauriana na wataalamu wetu"

"Ninaelewa, walioathiriwa na corona sijaona mwanamichezo yeyote aliyeathirika sana kwenye hili. Na hii inadhihirisha wazi kwamba kwa wale wanaofanya mazoezi corona inawakwepa"

"Sasa kama tunawazuia wasicheze mpira ina maana tunawaambia waugue corona," amesema Rais Magufuli

Kauli hiyo ya Mh Rais ni wazi itakuwa imekata mzizi wa fitina kuhusu hatma ya ligi kwani amebainisha kuwa ataruhusu iendelee

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
16h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’