Simba yasubiri kauli ya TFF hatma ya ubingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 May 2020
Simba yasubiri kauli ya TFF hatma ya ubingwa

Kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, matumaini ya ligi kuu ya Vodacom kurejea yanazidi kufifia kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona kuwa bado ni tatizo duniani

Wadau wa soka nchini wanasubiri kauli ya wasimamizi wa soka Tanzania (TFF) ambao wameeleza kusubiri muongozo wa Serikali

Baadhi ya nchi barani Afrika wakiwemo majirani zetu Kenya, wamechukua uamuzi wa kumaliza msimu kutokana na ukweli kuwa huenda janga la corona likaendelea kuisumbua dunia kwa muda mrefu zaidi

Kama ilivyo kwa wadau wengine, Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa, amesema wanasubiri kauli ya TFF kujua mustakabali wa ligi

Hata hivyo amesema TFF wanapaswa kutoa kauli mapema wasikae kimya kwa muda mrefu

"Sisi hatuna la kuzungumza, tunasubiri kauli yao. Wanatakiwa kuitisha Kikao cha Bodi ya ligi ambacho ni vyema kiwashirikishe viongozi wa klabu zote"

"Kikao hicho kitoe msimamo wa pamoja juu nini kifanyike kama zilivyofanya nchi nyingine ambazo tayari zimechukua maamuzi," amesema

Nae msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema anaamini kwa uamuzi wowote utakaotangazwa, ni lazima uwape klabu ya Simba haki wanayostahili

"Kwa uamuzi wowote utakaochukuliwa sisi tutaendelea kubaki namba moja. Kama ligi ikifutwa leo bingwa ni sisi, wakisema tucheze mechi zilizobaki bado bingwa atakuwa ni sisi na hata wakisema wafute wachukue matokeo ya msimu uliopita bingwa ni sisi"

"Jambo hili halipaswi kuchukua muda mrefu kwani kila litu kipo wazi," alisema Manara

Inaelezwa Kamati ya Utendaji ya TFF inatarajiwa kukutana wakati wowote kujadili mustakabali wa ligi baada ya Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF) kuwatumia wanachama wake waraka unaowaelekeza waweke wazi msimamo wao kuhusu hatma za ligi za nchi zao katika kipindi cha siku saba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’