Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa ufanyaji mazoezi wa wachezaji wake wakati huu ambao ligi imesimama kutokana na janga la corona
Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema wachezaji wake wamekuwa wakitekeleza kwa ufahasaha program ya mazoezi ambayo wanapaswa kufanya
Sven amesema alitoa program mbili za mazoezi, binafsi na mazoezi ya timu
"Utaratibu wetu wa mazoezi uko hivi, siku ya Jumatatu na Alhamisi wachezaji wanafanya mazoezi binafsi. Jumanne, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi wachezaji wote wanafanya mazoezi ya timu nzima kila mmoja huko aliko"
"Nafurahi kuona program zinakwenda vizuri, nadhani hatutakuwa na changamoto kubwa pale ligi itakaporejea," amesema
Bado hatma ya ligi iko mikononi mwa TFF ambayo inasubiri mwongozo wa Serikali kubainisha ni lini ligi hiyo inaweza kurejea au msimu huu kufutwa