Kwa sasa Waislamu kote duniani wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ibada hiyo ikifanyika wakati ambao dunia inakabiliana na janga la corona
Mshambuliaji kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba Meddie Kagere yuko kwao Rwanda, akitekeleza ibada hiyo ambayo ni lazima kwa kila Muislamu mwenye akili na afya timamu
Kagere amesema pamoja na kuwa katika ibada hiyo, anaendelea na program nyingine ikiwemo kufanya mazoezi ili kuendelea kujiweka 'fit'
"Siku yangu inaanza kwa kushiriki ibada ya kufunga, kuswali na baadae kufanya mazoezi ya viungo kwa lengo la kujiimarisha na kujiweka tayari kwa kumalizika msimu wa 2019/20," amesema
Mshambuliaji huyo alisema baada ya hapo programu yake inayofuata ni kuangalia filamu na humaliza na kitendo cha kupumzisha mwili wake kwa kulala
"Ninafanya kile ambacho nimepanga, hii ni kuniandaa na ligi ambayo bado msimu haujamalizika," alisema Kagere