Mambo yamemnyookea Salamba Kuwait

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 May 2020
Mambo yamemnyookea Salamba Kuwait

Mshambuliaji wa zamani wa Simba Adam Salamba anacheza klabu ya Al Jahra Sc inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Kuwait

Katika mahojiano aliyofanya Mwanahabari Shaffih Dauda, Salamba amesema Katika msimu wa ligi hiyo, klabu yake inaongoza ligi kabla ya kusimama kutokana na janga la Corora

Wamecheza mechi 13 na Salamba akiwa amefunga mabao sita (6) kwenye ligi na mawili (2) kwenye mechi za kirafiki na kufanya jumla ya mabao nane (8) tangu ajiunge na klabu hiyo.

Salamba anasema klabu ya Al Jahra ilianza kumfatilia muda mrefu tangu alipokuwa Uturuki akiwa na klabu ya Simba kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2018/19 na kocha wa timu hiyo kwa pamoja walionesha nia ya kumuhitaji kwenye timu yao ndio maana aliamua kujiunga na klabu hiyo kuliko kwenda sehemu nyingine

Salamba alijiunga na Simba mwaka juzi akitokea klabu ya Lipuli Fc. Alishindwa kutamba kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kwenye msimu wake wa kwanza kutokana na uwepo wa washambuliaji wakali zaidi yake John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi

Simba ilimtoa kwa mkopo klabu ya Namungo Fc mwanzoni mwa msimu huu kabla ya kuridhia kumuuza Al Jahra ambako alisaini mkataba wa miaka mitano

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’