Corona inaweza kuathiri huduma za wadhamini - Senzo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 May 2020
Corona inaweza kuathiri huduma za wadhamini - Senzo

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingisa amesema changamoto ya ugonjwa wa corona ambayo imepelekea shughuli zote za michezo kusitishwa, imewaweka wadhamini wa vilabu kwenye wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao

Barani Ulaya imeshuhudiwa vilabu vikichukua hatua ya kupunguza mishahara ya wachezaji wao ili kuweza kumudu gharama za uendeshaji baada ya makampuni yanayodhamnii vilabu hivyo kuathirika kiuchumi kutokana na corona

Senzo amesema wamejipanga kuiendesha klabu ya Simba kuhakikisha inavuka salama kipindi hiki ambacho kampuni nyingi zimeathiriwa

"Tulichonacho kama uongozi kipindi hiki ni kubaki na matumaini kwamba wadhamini watakwenda kutekeleza majukumu ya mikataba yao"

"Kwa maana hiyo ngoja tuone kwa upande wetu ni namna gani ambavyo tunajipanga ili kuweza kuendesha timu kipindi hiki ambacho sekta nyingi zimeguswa," amesema Senzo

Moja ya wadhamini wa klabu ya Simba ni kampuni ya SportPesa ambayo hujishughulisha na biashara wa ubashiri wa matokeo hasa ya mechi za mpira wa miguu

SportPesa ni miongoni mwa kampuni zilizoathirika kwa kiasi kikubwa baada ya ligi zote kubwa duniani kusimama kutokana na janga la corona

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’