Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amesema kuwa mlinda lango mwanzake Beno Kakolanya amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipojiunga na mabingwa hao wa nchi msimu huu
Manula ambaye ni chaguo la kwanza langoni mbele ya kocha Sven Vandenbroeck, ameeleza kuwa na wakati mzuri kufanya kazi na Kakolanya, wote kwa pamoja wameisaidia Simba kufanya vizuri

Amesema kuwepo langoni mara kwa mara haimaanishi kuwa yuko bora zaidi kuliko golikipa mwenzake
"Beno ni kipa mzuri na anafahamu kazi yake vilivyo, hilo ni jambo jema kwani linaifanya Simba kuwa salama na kufikia malengo. Nimekuwa chaguo la kocha kwa kupata nafasi mara nyingi, lakini haipotezi maana kuwa Kakolanya ni kipa mzuri na muda wote yuko tayari kusaidia timu kupata matokeo," amesema
Kakolanya alijiunga na Simba akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Yanga kutokana na malimbikizo ya madeni aliyokuwa akiidai klabu hiyo