Djuma afunguka alivyoamsha mzuka wa Gyan

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jan 2018
Djuma afunguka alivyoamsha mzuka wa Gyan
Kama ulikuwa hujui, kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma alipojiunga na Simba tu, alimtamkia Mghana Nicholas Gyan kuwa hajui mpira na si mchezaji lakini anachoshukuru kiraka huyo alimjibu kwa vitendo.

Djumba ambaye ni msema ukweli na hapendi kuficha mambo amesema, baada ya kujiunga na Simba alimkuta Gyan anacheza nafasi ya ushambuliaji lakini hapigi pasi wala hazimi.

"Nilimwita Gyan na kuzungumza naye na nikamwambia wewe si mchezaji, inakuwaje haupigi pasi, wala hauzimi kwa sababu haiwezekani mchezaji awe anakosa vitu hivyo, lakini kumbe mwenyewe kichwani alikuwa na akili yake kuwa anarogwa,"anasema Djuma.

"Aliamini kuwa anashindwa kucheza mpira kwa sababu analogwa, kwa sababu alipokuwa kwao Ghana alikuwa mchezaji mzuri wa kiwango cha taifa, nikakaa naye na kumtengeneza kisaikolojia nikampa nafasi ndiyo kama unamwona anafanya vizuri ndivyo ilivyokuwa."

Hata hivyo, katika kumpa nafasi mchezaji huyo, Djuma alimpanga kucheza pembeni upande wa kulia kama beki namba mbili anayepanda kutokana na mfumo wake wa 4-4-2 unaobadilika kuwa 3-5-2 kiuchezaji.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
57m ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
15h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
18h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’