Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroec amesema kuwa hana tatizo na kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu na anaamini anaweza kuwa bora baadaye ikiwa ataongeza juhudi kwenye mazoezi.
Ajibu ametua Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa akitokea Klabu ya Yanga ambayo alicheza misimu miwili akitokea Simba.
Sven ameeleza kuukubali uwezo wa fundi huyo wa mpira lakini amemtaka ajitume zaidi katika mazoezi ili aweze kufika mbali
"Ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa kwani kuna mechi nilikuwa ninampa nafasi na alikuwa anatimiza majukumu yake vizuri sina tatizo naye kabisa"
"Kikubwa nimekuwa nikimwambia afanye mazoezi kwa juhudi ili kuzidi kuwa bora," Sven amenukuliwa na mtandao wa Salehjembe
Tangu arejee Msimbazi, Ajibu amaefunga bao moja na kutoa pasi nne za mabao
Msimu uliopita Ajibu alikuwa kinara wa kutoa pasi za mabao ligi kuu ya Tanzania bara, akitoa pasi 17 na mwenyewe akiweka kambani mabao saba, wakati huo akiitumikia Yanga