Uongozi wa klabu ya Azam umesema hauna mpango wa kumuuza mlinzi wao Yakub Mohammed raia wa Ghana
Kumekuwa na tetesi kuwa Bilionea Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' alitaka kumvuta beki huyo mahiri Msimbazi
Mtendaji wa Azam Fc Abdulkarim Amin amesema hawana mpango wa kumuuza beki huyo ambapo amesema bado ana mkataba wa miaka miwili
"Tumezisikia taarifa za Simba kumtaka mchezaji wetu, lakini nawaambia wasijisumbue kwa kuwa hatuna mpango wa kumuuza. Yakub bado ana mkataba wa miaka miwili nasi hivyo hawezi kupatikana wakati huu," alisema Amin
Simba imedhamiria kusajili mlinzi wa kati wa daraja la juu ambaye ataongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa nchi
ADVERTISE HERE