Mtibwa Sugar yamtamani Kichuya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Apr 2020
Mtibwa Sugar yamtamani Kichuya

Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umeonyesha kumnyemelea winga wa Simba Shiza Kichuya ambaye amerejea Msimbazi katika usajili wa dirisha dogo mwezi Januari 2020

Kichuya alisajiliwa na Simba mwaka 2016 akitokea klabu ya Mtibwa, alifanya mambo makubwa Msimbazi kabla ya kupata dili la kwenda kucheza soka nchini Misri msimu uliopita

Hata hivyo Simba ilimrejesha tena Msimbazi mwaka huu

Tangu kurejea nchini, Kichuya amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba huku ikielezwa kuwa kocha Sven Vandenbroeck bado hajavutiwa na kiwango chake

Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru, amesema kama nyota huyo atarejea Manungu, watamrudisha katika ubora wake kama ilivyokuwa kwa Hassan Dilunga ambaye kwa sasa anatamba Msimbazi

"Kichuya ni mwanangu kama atataka kurudi nyumbani tunamkaribisha, hiki ni Chuo cha Tanzania akishindwa maisha ya huko aliko tunamkaribisha, tunampa mwezi mmoja atanolewa na atakuwa bora kuliko yule Kichuya wa mwanzo, " amesema

Kifaru alimtolea mfano mmoja wa wachezaji waliowahi kuonekana hawafai baada ya kucheza klabu mbalimbali kuwa ni Hassan Dilunga lakini aliporejea Mtibwa akatengenezwa na kurudi mpya na leo amekuwa ni mmoja wa wachezaji hatari kwenye kikosi cha Simba.

Pia alisema wachezaji wengi wakirudi kwenye klabu hiyo wanafanikiwa kwa sababu wamefanya uwekezaji mkubwa na wana kila kitu kinachohitajika kwenye soka tofauti na klabu nyingine.

Aidha Kifaru aliongeza kuwa Kichuya akirudi atapewa programu maalumu na kocha wao na yeye kama mzazi pia atampa maneno yatakayomjenga.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’