Ajib aendelea kutoa misaada kujikinga na Corona

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Apr 2020
Ajib aendelea kutoa misaada kujikinga na Corona

Kiungo wa Simba, Ibrahim Ajibu, amekuwa mchezaji wa kwanza nchini kutoa msaada binafsi kwa wahitaji katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na janga la ugonjwa wa COVID-19, unaosababishwa na virusi ya corona

Juzi, Ajibu alitoa msada kwa watoto yatima kwenye Kituo cha Umra kilichopo Magomeni Mikumi na Mayunga kilichopo Kinondoni Moscow, vyote vya jijini Dar es Salaam.

"Mimi Ajibu mchezaji wa Simba, kama Mtanzania, nimeguswa sana na janga lililotukabili kwenye nchini yetu na dunia kwa jumla la ugonjwa wa corona. Nimeamua kuanzisha kampeni hii ya kuisaidia jamii na watoto yatima, kwenye kampeni hii ya kujitolea, vifaa kama sanitizer [vitakasa mikono], ndoo za kunawia mikono, pamoja na chakula," Ajib amenukuliwa na gazeti la Nipashe

"Pia ningependa kutoa hamasa kwa wadau wengine ili kujiunge na mimi kufanikisha zoezi hizi."

Ajibu alisema kuwa hiyo si mara ya kwanza kwake kugawa misaada kwa watoto yatima, kwani ni sehemu ya maisha yake kufanya hivyo mara kadhaa.

"Nitakuwa nikiendelea kutoa kadri Mungu atakavyokuwa ananijaalia, nitakuwa nagawana na watoto yatima, kutegemeana na kipato changu," alisema.

Kujitolea kwa mchezaji huyo kumezua mjadala mkubwa mitaani kwa wadau wa soka kuwataka baadhi ya wachezaji wa Kitanzania vipenzi vya mashabiki kuiga mfano wake huku pia klabu kongwe nchini Simba na Yanga zikitakiwa kutobaki nyuma katika kipindi hiki kigumu ambacho taifa linakabiliwa na janga hilo la corona.

Kwa upande wa klabu ya Simba Ajibu ni mchezaji wa pili kufanya hivyo, baada ya Mkenya Francis Kahata kugawa lita 10,000 za maji kwa jamii inayomzunguka nyumbani kwao jijini Nairobi wakati huu wa janga la corona.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’