Meneja wa klabu ya Simba Patrcik Rweyemamu amesema wanafuatilia mazoezi ya wachezaji wao kipindi hiki ambacho ligi imesimama kutokana na janga la corona
Benchi la ufundi la Simba lilitoa program maalum ya mazoezi kwa wachezaji ambayo wanapaswa kuyafanya majumbani kwao
Rweyemamu amesema wachezaji watakaporejea kambini, watajiridhisha kama walikuwa wakifanya mazoezi inavyotakiwa
"Tumekuwa na utaratibu wa kuwafuatilia wachezaji wetu kupitia makundi yetu ya mitandao ya kijamii kuona wanavyotekeleza program za mazoezi tuliyowapa"
"Watakaporejea tutajiridhisha kuona kama walikuwa wakifanya mazoezi sawasawa, moja ya mbinu tutakayotumia ni pamoja na kuwapima uzito. Ni muhimu kwa kila mchezaji kufanya mazoezi kwani ligi itakaporejea tunaweza tusiwe na muda mrefu wa maandalizi na mechi zinaweza kuchezwa mfululizo hivyo kama wachezaji hawatakuwa 'fit' linaweza kuwa tatizo," alisema
Hata hivyo wachezaji wengi wa Simba wamekuwa wakitekeleza program za mazoezi kikamilifu baadhi wakitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kutupia picha na video za mazoezi wanayofanya