Bado mapema kufikiria kumaliza msimu - TPLB

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Apr 2020
Bado mapema kufikiria kumaliza msimu - TPLB

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amesema kwa sasa ni mapema mno kufikiria kumaliza msimu kutokana na janga la corona, lakini pia maamuzi yoyote yatatolewa na kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)

Hivi karibuni kumeibuka mjadala baada ya baadhi ya wadau kupendekeza ligi imalizwe na klabu ya Simba inayoongoza ligi hiyo kupewa ubingwa

Bosi huyo wa Bodi ya Ligi amesema hakuna kanuni yoyote inayoelekeza hatua za kuchukuliwa pale ligi inaposhindikana kufika mwisho hivyo uamuzi wowote utaamuliwa na kikao cha Kamati ya Utendaji kwa kuwashirikisha wadau

Aidha Kasongo amesema ni wakati TFF na wadau wake kukaa chini kutengeneza kanuni ambayo itaepusha sintofahamu juu ya hatua za kuchukuliwa pale ligi inapokwama

"Kanuni hazisemi linapotokea janga kama hili nini kifanyike, zinazungumzia tu mchezo. Pengine ni wakati mwafaka kufanya maboresho ya kanuni baada ya janga hili," amesema

Hata hivyo Rais wa TFF Wallace Karia amesema kwa sasa hakuna hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa hadi hapo Serikali itakapotaoa mwongozo wake

Kumekuwa na makundi tofauti miongoni mwa wadau wanaopendekeza nini kifanyike kama ikitokea ligi haitawezekana kumalizika

Kundi la kwanza ni wale wanaotaka timu inayoongoza ligi ipewe ubingwa kisha kuwe na mechi chache za 'play-off' kusaka nafasi ya pili na timu za kushuka daraja

Kundi jingine linataka subira iendelee kutawala ili mambo yatakapotulia basi ligi iweze kuendelea. Hata hivyo changamoto hapa ni muda kwani inawezekana jambo hilo likachukua muda mrefu pengine hata kuathiri muda wa kuanza msimu ujao

Lakini pia wapo wanaopendekeza mechi za playoff zichezwe kutafuta bingwa wa ligi kuu na timu zinazopaswa kushuka daraja huku kundi jingine likipendekeza msimu mzima ufutwe kama ilivyofanya nchi ya Uholanzi

Uamuzi huo pia uhusishe ligi daraja la kwanza, la pili na madaraja mengine ili msimu ujao timu zote zianze upya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’