Beki kiraka wa Simba Erasto Nyoni amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona ambao umeendelea kuwa tishio duniani
Nyoni amesema anafahamu kila mmoja ana shauku ya kuona mambo yanakuwa sawa na ligi kuendelea lakini kwa sasa ni muhimu kulinda afya na uhai wa kila mmoja wetu kutokana na janga hilo
"Tunapaswa kufuata maelekezo tunayopewa na wataalam. Kama huna ulazima wa kutoka nyumbani kwako ni vyema ukabaki. Tusisahau kuvaa barakoa tunapotoka. Pia tunawe mikono au kutumia sanitizer mara kwa mara," amesema
"Mimi binafsi natumia muda mwingi nikiwa nyumbani huku nikichukua tahadhari dhidi ya Corona"
Mkongwe huyo ameanza mazoezi binafsi baada ya kupona majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Yanga ambao ulipigwa March 08