Maoni ya Manara kupunguzwa idadi ya nyota wa kigeni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Apr 2020
Maoni ya Manara kupunguzwa idadi ya nyota wa kigeni

Afisa habari wa klabu ya Simba nae amekosoa mapendekezo ya Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe aliyeliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuandaa kanuni itakayoweka ukomo wa idadi ya wachezaji wa kigeni wanaopaswa kusajiliwa nchini

Manara ameandika Makala hii;

TUNAJIANDAA KUKOSEA ZAIDI

Wakati huu janga la ugonjwa hatari wa Corona likiichachafya dunia, habari kubwa ya kispoti nchini ni kuhusiana na wazo la Mh Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Dr Harrison Mwakyembe la kutaka kupunguzwa kwa idadi ya wachezaji wa kigeni wanaocheza katika Ligi Kuu nchini, toka kumi wa sasa na kufikia watano

Hoja ya Waziri ni kuwa wachezaji wa kigeni wanawanyima wachezaji wetu wazawa fursa zaidi ya kucheza na hatimae kutokuwa na kikosi bora cha Timu ya Taifa.

Hapa ndio tunapojiandaa kukosea zaidi, maana huko nyuma tushakosea sana kiasi cha kwamba leo Tanzania sio nchi bora katika mchezo huo unaopendwa zaidi duniani, tumekosea Kwenye mipango yetu na maamuzi yetu kama hayo, lakini tunaona haitoshi na sasa tunajiandaa kukosea zaidi ili Tanzania isifanikiwe kisoka.

Ndio makosa yetu ni kuona Tanzania ni kisiwa na inaweza kuja na mikakati na mipango tofauti na tukaweza kuwa Bingwa wa Afrika na hata dunia.

Tunaweza kufuta mashindano ya vijana na watoto kote kuanzia ngazi za mtaani hadi mashuleni na tukawa na ligi bora duniani

Tunaweza kuviachia viwanja vya watoto kuwa makontena ya kuuzia pombe na bado tukawa na rundo la vikombe vya kimataifa

Tunaweza kugeuza viwanja vya Jangwani stand ya mabasi Na bado siku moja Tanzania ikamtoa Messi na Ronaldo kwa wakati mmoja, kiufupi Tanzania tunajua kuliko Misri au Ghana katika soka na tuna mipango mizuri kuliko hata Uholanzi , labda tunawazidi kidogo tu Morocco na Brazil

Wakati nchi nyingi zinategemea uzalishaji wa wachezaji wadogo katika vituo vyake imara vya mafunzo ili kuwa na timu bora ya taifa, sie tunafikiria kuwa na ligi ya wazawa watupu kina Makumbi Juma na Moses Mkandawile

Wakati nchi nyingine za kiafrika zinajitahidi kuwawekea mazingira rafiki na kutoa fursa zaidi kwa wachezaji wao kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya ili wawe na kikosi bora cha timu ya taifa, sie tunaona dawa ya timu imara ya taifa ya Tanzania ni kuwapunguza kina Kagere na Morrison na kuwaachia kina Tenende na Kayeta wawe peke yao ili tupate Taifa Stars ya ahadi

Sijui tunafeli wapi??

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’