Yakubu atajwa usajili Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Apr 2020
Yakubu atajwa usajili Simba

Inaelezwa uongozi wa klabu ya Simba uko kwenye mazungumzo na Azam Fc wakitaka saini ya beki kisiki wa timu hiyo Yakubu Mohammed raia wa Ghana

Yakubu amekuwa na kiwango kizuri kunako klabu ya Azam tangu aliposajiliwa na timu hiyo misimu kadhaa iliyopita

Katika jitihada za kuisuka upya safu ya ulinzi, mabosi wa Simba wametua kwa Mghana huyo ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Azam

"Ni kweli Simba inamtaka Yakubu, mazungumzo yapo lakini mpaka sasa bado hakuna makubaliano yaliyofikiwa lakini kama kila kitu kitaenda sawasawa, msimu ujao anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Simba," alifunguka mtoa taarifa ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani

Katika ripoti ya usajili iliyopendekezwa na Sven Vandenbroeck, Mbelgiji huyo ametaka kuongezewa walinzi wawili, mmoja wa kati na mwingine wa pembeni

Juzi Afisa Mtendaji wa Simba Senzo Mazingisa alisema kuwa hawana wasiwasi kuwapata wachezaji wanaowataka kwani wanalo fungu la kutosha

Alisema wanaweza kumsajili mchezaji yeyote anayecheza ndani, labda watapata changamoto kwa baadhi ya wachezaji wa nje ambao mara nyingi masharti yao huwa ni tofauti

Mazingisa alisema kwa sasa hawajaanza usajili wa wachezaji wapya, lakini wakati ukifika wataweka hadharani nyota wanaowasajili kama walivyofanya msimu uliopita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’