Ukizungumzia wachezaji mafundi wa mpira kwenye ligi kuu ya Vodacom pengine jina la Sharaff Elden Shiboub linaweza kuwa sambamba au chini ya Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka'
Shiboub aliyetua Simba kutoka klabu ya El Hilal ya Sudan ni mmoja wa wachezaji ambaye kumtazama akiwa dimbani ni burudani tosha
Hata hivyo tangu kutua kwa kocha Sven Vandenbroeck, Shiboub ni kama amepungua makali kwani haonekani mara kwamara kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa wakati wa Patrick Aussems
Shiboub amekiri kuwa kiwango chake kimetetereka kidogo hivyo amekuwa akifanyia kazi changamoto hiyo wakati huu ambao ligi imesimama ili kuhakikisha anarejea kwa nguvu pale itakaporejea kumalizia mechi zilizobaki
Shiboub kwa sasa yupo kwao Sudan akiendelea kujifua
"Nipo nyumbani kutoka na janga hili la Corona na sijui litaisha lini ili nirudi Tanzania kujiunga na timu yangu. Pamoja na hali hiyo, bado ninajifua sana huku ili niweze kuwafi ti na nitakaporudi Simba nipate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa zamani," amesema
"Kusema kweli hakuna jambo linaloniumiza kama kutocheza, kwa hiyo napambana huku kwa kufanya mazoezi ya nguvu ili niweze kuwa fiti na kocha atakaponiona basi asiwe na shaka tena na mimi"
Pamoja na kutopata nafasi kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, Shiboub ni miongoni mwa wachezaji wanaoongoza kwa kutoa 'asisti' ligi kuu ya Vodacom, akiwa ametoa pasi tano za mabao