Wakati huu ligi ikiwa imesimama kutokana na changamoto ya janga la corona, wachezaji wa Simba wametakiwa kujisimamia mazoezi wao wenyewe ili kuhakikisha wanakuwa 'fit' pale ligi itakaporejea
Jambo hilo ndilo linalomfanya kiungo fundi wa mpira, Ibrahim Ajib 'Mzee wa makorokoro' kujiongezea dozi ya mazoezi juu ya yale ambayo anapewa na kocha wake Sven Vandenbroeck
Ajib amefichua kuwa anafanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi akifanya mazoezi binafsi na jioni akitekeleza program aliyoachiwa na kocha wake

Ajib amekuwa na changamoto ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na vita ya namba hasa eneo la kiungo ambalo Simba imesheheni mafundi kwelikweli
Pengine kipindi hiki kinaweza kuwa mwafaka kwake kujiweka sawa ili kujihakikishia namba pale ligi itakaporejea