Ndayiragije atoa maoni idadi nyota wa kigeni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Apr 2020
Ndayiragije atoa maoni idadi nyota wa kigeni

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Etienne Ndayiragije ametoa maoni kuhusu mjadala wa kupunguzwa idadi ya nyota wa kigeni wanaocheza nchini ambapo amesema kama uamuzi huo utachukuliwa, unaweza kuwa na athari kwa kupunguza ushindani wa vilabu kwenye medani ya Kimataifa

"Soka sasa ni biashara ya Kimataifa. Unapojaribu kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye nchi yako ni kama unataka kufanya soka lako liwe 'loko'. Kutakuwa na athari timu zinapokwenda kushiriki michuano ya Kimataifa kwani maandalizi yako yatakuwa tofauti," amesema

"Kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni haiwezi kuwa suluhu ya kuinua viwango vya wachezaji wa ndani, jambo linaloweza kufanyika ni kuwahimiza wachezaji wazawa nao wapambane ili wapate nafasi ya kwenda kucheza soka nje"

"Leo hii mngekuwa na wachezaji wengi wanacheza mfano ligi kuu ya Uingereza msingeleta huu mjadala wa kupunguza idadi ya nyota wa kigeni wanaocheza hapa," aliongeza Ndayiragije

Hivi karibuni Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe aliliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuunda sheria ambayo itaweka ukomo wa idadi ya nyota wa kigeni wanaosajiliwa na vilabu nchini

Dk Mwakyembe alisema kama kukiwa na ukomo, vilabu vitakuwa makini katika kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi kwani kwa utaratibu wa sasa, wengi wanaosajiliwa wanakosa ubora

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’