Ligi Kuu bado imesimama kutokana na changamoto ya janga la corona huku hatma yake ikiwa kizani
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linasubiri mwongozo wa Serikali ikiwa ni baada ya Serikali kusitisha shughuli zote za michezo kwa muda usiojulikana mpaka pale corona itakapokuwa imedhibitiwa nchini
Baadhi ya wabunge wameishauri Serikali kumaliza msimu huu kwa kuwapa Simba ubingwa ili kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Lakini pia wamependekeza Azam Fc ambao wako nafasi ya pili, wapewe nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho kwa kuwa ndio mabingwa watetezi kombe la FA
Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo alisema kwa sasa mkakati walionao ni kuhakikisha ligi inamalizika kwa mechi zilizobaki kuchezwa lakini ikitokea tofauti, wadau wa soka watashirikishwa ili kupata mwafaka wa nini kifanyike