Baada ya Dilunga, Mzamiru, Wawa kufuata

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Apr 2020
Baada ya Dilunga, Mzamiru, Wawa kufuata

Mwekezaji wa Simba, bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ameonekana kupania kuwabakisha mastaa wake wote muhimu wanaomaliza mikataba yao, na sasa ni zamu ya kiungo mkabaji Mzamiru Yassin na beki Muivory Coast Pascal Wawa ambao wapo kwenye mazungumzo ya mwisho kukamilisha usajili wao.

Mo tayari amefanikiwa jaribio la Kampuni ya GSM iliyopo kwenye mipango ya kukamilisha usajili wa kiungo wao mshambuliaji Hassan Dilunga ambayo ilimtengea dau la Sh milioni 80 ili asaini mkataba wa kukipiga Jangwani kwenye msimu ujao.

Mzamiru ni kati ya wachezaji wengine watano ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, wengine ni Wawa, Shiza Kichuya, Sharraf Eldin Shiboub, Yusuph Mlipili na Dilunga.

Inaelezwa hivi karibuni Mzamiru alifanya mazungumzo na Bodi ya Wakurugenzi wa Simba inayoongozwa na Mo kwa ajili ya kuhakikisha anaongeza mkataba mpya wa kukipiga Msimbazi

Aliongeza kuwa tayari mazungumzo yanakwenda vizuri na huenda kiungo huyo akasaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Simba kama ilivyokuwa kwa Dilunga ambaye muda wowote ataongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo.

"Kwa mujibu wa ripoti ambayo kocha Sven (Vandenbroeck) aliitoa kwa viongozi, Mzamiru ataendelea kuwepo kwenye usajili wa msimu ujao, hivyo tayari viongozi wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mipango hiyo ya kumbakisha.

"Wapo wachezaji wengine ambao tayari viongozi wameanza mazungumzo nao ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu na hiyo yote ni katika kuepukana na presha mwishoni mwa msimu kutoka kwa timu pinzani watakaowahitaji wachezaji hao.

"Baada ya Dilunga dili lake kukamilika hivi sasa viongozi wamegeukia kwa Mzamiru ambaye yeye mwenyewe ameonyesha nia ya kubakia Simba, kama mambo yakienda sawa atapewa mkataba kwa ajili ya kuupitia,” alisema mtoa taarifa huyo"

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’