Wawa hahitaji mpishi kwake, mtaalamu mwenyewe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Apr 2020
Wawa hahitaji mpishi kwake, mtaalamu mwenyewe

Beki wa Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast amefichua kuwa kwa sasa amekuwa akitumia muda mwingi katika upishi kwa kujipikia vyakula anavyopenda kila baada ya kumaliza mazoezi kutokana na kuwepo kwa Ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona.

Wawa ametoa kauli hiyo kutokana na kitendo chake cha kuonyesha video zake katika mitandao ya kijamii akiwa anapika vyakula vyenye asili ya kwao kila baada ya kutoka mazoezini.

 Beki huyo mkongwe amesema kuwa kwa sasa anatumia muda wake kufanya mazoezi binafsi na kupika tu kutokana na kuwa ni mambo anayopenda kufanya

"Kiukweli napenda kupika, napenda sana ndiyo maana umeona hizo video nikiwa naandaa chakula changu ninachopenda na inakuwa inanipa urahisi wa kujua nini nataka kula"

"Unajua suala la kupika kwangu ni jambo la kawaida kwa sababu nimekuwa nikipenda kufanya hivyo na kwa sasa nimekuwa nikifanya mazoezi halafu nageukia mapishi hakuna kitu kingine cha kufanya kwa sababu ya Corona ambayo imezuia kila kitu," alisema Wawa

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’