Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema Mzambia Clatous Chama, kiungo mshambuliaji, amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya kikosi chake msimu huu
Chama ndiye kinara wa pasi za mabao ligi kuu ya Vodacom akiwa ametoa pasi nane zilizozaa mabao
Hivi karibuni alitawala sana kwenye vyombo vya habari baada ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela kudai timu yake ilikuwa kwenye mpango wa kumsajili kauli ambayo ilimuingiza matatani kiongozi huyo
Ni baada ya uongozi wa Simba kupeleka malalamiko TFF wakiituhumu klabu ya Yanga kuvunja taratibu za usajili kwani Chama bado ana mkataba wa zaidi ya miezi sita na mabingwa hao wa nchi
Sven amesema hakutishwa na tetesi zilizokuwa zikimuhusisha nyota huyo na Yanga kwani anafahamu mchezaji wa mpira wa miguu anaweza kwenda kucheza popote
Hata hivyo amesema anafurahi kufanya kazi na Chama kwani mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi chake
"Kwa kumzungumzia Chama, ni mchezaji mzuri, kwa sasa bado ni mchezaji wetu na amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yetu"
"Anapokuwa uwanjani ana uwezo wa kubadili matokeo muda wowote. Amekuwa akifanya vizuri na nafurahi kuwa nae," amesema
Chama yuko kwao Zambia akiendelea na akiendelea na mapumziko baada ya ligi kusimama kutokana na changamoto ya janga la corona