Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba, Crescentius Magori, amesema kabla ya klabu hiyo kuanza kufikiria taji la ligi ya mabingwa, inapaswa wajenge utamaduni wa kucheza hatua ya makundi kila msimu
Magori ambaye wakati akiwa Mtendaji Mkuu aliwaongoza mabingwa hao wa nchi hadi kufika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika kwa ngazi ya vilabu, amesema huo unapaswa uwe utamaduni wa Simba
"Utatakiwa kujihakikisha kuingia mara kwa mara katika makundi, halafu robo fainali, hapo tayari utakuwa unafikiria ubingwa wa Afrika, tunahitaji kuendelea kuwekeza, kwa kuanzia kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kupambana kwenye hatua hizo za juu," amesema.
Simba iko katika mkakati wa kukiimarisha kikosi chake ili kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara kwani waliondoshwa kwenye hatua za awali