Simba ndio sehemu sahihi kwa mchezaji anayetaka mafanikio makubwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Apr 2020
Simba ndio sehemu sahihi kwa mchezaji anayetaka mafanikio makubwa

Beki wa kushoto wa Simba Gadiel Michael amefichua kuwa kilichomsukuma kuachana na klabu ya Yanga na kujiunga na mabingwa wa nchi, ni kiu ya kushinda mataji na kucheza mashindano makubwa

Siku ya jana haikuwa nzuri kwa beki huyo mahiri baada ya kufiwa na Baba yake Mzazi. Tunampa pole, Mwenye ez Mungu ampe uvumilivu katika kipindi hiki kigumu

Hata hivyo juzi wakati akihojiwa na mashabiki kwenye kipindi cha ChatNa, Gadiel alifichua sababu iliyompeleka Simba

"Ukiangalia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Simba, naamini katika kipindi cha miaka 10 klabu itakuwa mbali sana.

"Mimi kama mchezaji nina malengo, hivyo niliangalia na kuona hapa ni mahali sahihi ambapo ninapaswa kuwepo.

"Nilijiunga na Simba wakati timu ikiwa imepata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa. Michuano hii inaweza kuwa sehemu ya kukufanya uonekano zaidi na pengine kupata nafasi ya kwenda kucheza soka nje ya nchi," alisema

"Sijutii kujiunga na Simba kwani naamini niko sehemu sahihi ambapo ntaweza kufikia malengo yangu"

Gadiel ni mmoja wa wachezaji watatu waliojiunga na Simba mwanzoni mwa msimu wakitokea klabu ya Yanga

Wengine ni Ibrahim Ajib aliyekuwa nahodha wa Yanga na mlinda lango Beno Kakolanya ambaye alivunja mkataba wake na timu hiyo baada ya Yanga kushindwa kumlipa mishahara

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’