Ujumbe wa Gakumba kwa wanaombeza Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Apr 2020
Ujumbe wa Gakumba kwa wanaombeza Kagere

Patrick Gakumba ambaye ni Wakala wa mshambuliaji nyota wa Simba Meddie Kagere, amesema mteja wake atacheza hadi watoto wadogo wanaomuita mzee watoke na kumuacha akiendelea kucheza

Gakumba amesema alianza kusikia muda mrefu Kagere akiitwa Mzee lakini kazi yake anayoifanya uwanjani imemfanya asakwe kila mahali

"Tangu wameanza kumsema Kagere amezeeka miaka mitano imepita, na kila wanavyoendelea anafunga"

"Ninachoangalia ni mabao siangalii umri, nilisema sihitaji kumleta mchezaji ambaye ataniaibisha na heshima yangu ikashuka kisa ana umri mdogo," alisema Gakumba

Hivi karibuni Gakumba alidai kuwa klabu ya Levante inayoshiriki ligi kuu ya Hispania, La Liga ilimuuliza mshambuliaji huyo ikitaka kumpa mkataba wa miezi sita

Hata hivyo amesema alikataa dili hilo la muda mfupi akitaka mteja wake apewe mkataba wa kuanzia miaka mawili

Gakumba amesema wako kwenye mazungumzo na uongozi wa Simba kwa ajili ya mkataba mpya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’