Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema klabu yake haina taarifa kuhusu Levante kumtaka mshambuliaji wao Meddie Kagere
Hivi karibuni wakala wa mchezaji huyo Patrick Gakumba alidai kuwa klabu ya Levante iliwasialiana nae kumtaka mshambuliaji huyo
Gakumba alidai kuwa Levante walikuwa tayari kumpa Kagere mkataba wa miezi sita lakini yeye alikataa
"Hakuna kiongozi yeyote anayefahamu taarifa hizi na hakuna muda wa kufutilia jambo hili ambalo linapoteza muda inakuwaje watu kuwa na taarifa za wachezaji wetu huku klabu haijui lolote au Levante kusambaza taarifa hizi bila kuwasiliana na uongozi wa klabu," amesema Mazingiza.
Aliwataka mashabiki wa Simba kuacha kufuatilia taarifa ambazo hazijathibitishwa na uongozi hasa katika kipindi hiki ambacho kuna tetesi nyingi zisizo na ukweli zinazoibuliwa na watu wasiotaka kuona klabu yao inapiga hatua kimaendeleo.