Inaelezwa uongozi wa Simba umemalizana na kiungo wake mshambuliaji Hassan Dilunga ambaye amekubali kusaini mkataba wa kuendelea kucheza Msimbazi wa misimu mingine miwili
Nyota huyo aliyeifungia Simba mabao saba kwenye ligi msimu huu, amekuwa akihusishwa na timu kadhaa vikiwemo vilabu kutoka nchi za Misri na Afrika Kusini
Hapa nchini alikuwa akitajwa kuwaniwa na vilabu vya Azam Fc na Yanga ingawa mwenyewe alikanusha tetesi za kujiunga na Yanga akiweka bayana kuwa kama angekosa mkataba Simba ni bora angerejea Mtibwa Sugar ambako ndiko alipotengeneza jina lake
Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema kwa sasa wanaendelea na mazungumzo ya wachezaji waliopendekezwa na kocha waendelee kubaki ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu
ADVERTISE HERE