Tunawatamani kwelikweli Yanga - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Apr 2020
Tunawatamani kwelikweli Yanga - Manara

Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema wako tayari kucheza na Yanga hata leo hii kama isingekuwa changamoto ya virusi vya COVID-19 vinavyosababisha ugonjwa wa corona

Kumekuwa na maoni ya wadau waliopendekeza kuwa iwapo ligi itashindwa kumalizika kutokana na changamoto ya corona, njia rahisi inayoweza kuchukuliwa ni kupunguza idadi ya mechi kwa ligi kumalizwa kwa mtindo wa 'Play-Off' utakaozikutanisha timu zinazowania ubingwa na zile zinazopambana zisishuke daraja

Akitoa maoni yake kuhusu mapendekezo hayo, Manara amesema haamini kama TFF itafanya maamuzi ya kutumia utaratibu huo. Muhimu kwa sasa ni kuendelea kuomba Mungu ili jitihada zinazofanywa na Serikali katika mapambano ya corona zifanikiwe ili mechi zote zilizobaki zichezwe na bingwa apatikane kwa utaratibu wa kawaida

Lakini amesema hata ikitokea TFF wakatumia utaratibu huo, wako tayari kucheza na timu yoyote ikiwemo klabu ya Yanga ambayo msimu huu wamekutana nayo mara mbili bila kupata ushindi dhidi yao

"Sisi ndio tuko kileleni mwa msimamo wa ligi kwa pointi nyingi, tunawezaje kuihofia timu yoyote ambayo iko chini yetu?," alihoji Manara

"Tena hao Yanga dio tunawatamani kwelikweli kwani katika mechi tulizokutana nao walikuwa na bahati tu. Nimeona maoni mengi ya wachambuzi hapa nchini wanadai katika mchezo uliopita waliotufunga, wanasema wao walicheza vizuri kuliko sisi, jambo hili sio kweli"

"Katika mchezo ule, nyota wa mchezo alikuwa kipa Metacha Mnata, sisi tulikosa nafasi saba za wazi wakati wao walitengeneza nafas mbili tu. Tunajua tunaweza kukutana nao tena kwenye FA, tunawasubiri kwa hamu.." alitamba Manara

Msimu huu Yanga ilijitutumua na kuweza kuondoka na ushindi kwenye mchezo uliopigwa March 08 ikiwa ni mara ya kwanza kuifunga Simba tangu mwaka 2015..!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’