Idadi ya walioambukizwa corona yafika 147

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Apr 2020
Idadi ya walioambukizwa corona yafika 147

Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu amethibitisha visa vipya 53 vya ugonjwa wa corona na hivyo kufanya idadi ya watu walioathirika na ugonjwa huo kufikia watu 147

Katika taarifa aliyotoa kwa Wanahabari mapema leo,Β  Mh Ummy amesema kwamba wagonjwa wote ni raia wa Tanzania.

Amesema kwamba kati ya wagonjwa hao kuna watu 38 kutoka mkoa wa Dar es salaam, Kisiwani Zanzibar watu 10, Kilimajanro mtu 1, Mwanza mtu 1, Pwani Mtu 1 na Kagera mtu 1

"Mnaweza kuona nimetoa takwimu kubwa sana lakini tumeamua tuseme ukweli kwa sababu watanzania sasa lazima waelewe kuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa"

"Kama kuna mmoja alikuwa na shauku basi ni wakati afahamu Corona inaanza na wewe kujikinga na pia uwakinge wengine," amesema Waziri

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutangazwa kwa siku moja tangu mgonjwa wa kwanza kugundulika nchini

Waziri Ummy amewataka Watanzania kuendelea kujihadhari na ugonjwa huo ambao umeendelea kuwa changamoto kwa Mataifa yote duniani

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
56m ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
15h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
18h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’