Simba mpya ni baada ya miezi minne

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Apr 2020
Simba mpya ni baada ya miezi minne

Kamati ya kuratibu mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ya Simba imewahakikishia Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kuwa michakato yote itakuwa imekamilika katika kipindi cha miezi minne kuanzia sasa

Mmoja wa wajumbe wa kamati inayosimamia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo, Mulamu Nghambi amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti akisema kuwa mpaka sasa klabu ya Simba imekwisha sajili kampuni yake, Simba Holding Limited ambayo inamilikiwa na wanachama.

Nghambi amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu, kampuni hiyo imesajiliwa Brela na ni mali ya wanachama wa klabu hiyo huku mwekezaji, Mo Dewji naye amekwisha kamilisha usajili wa kampuni ambayo itawekeza ndani ya klabu hiyo ijulikanayo kwa jina la Mo Simba Holding Limited

"Kampuni ambayo itaendesha klabu ya Simba, Simba Sports Club Limited nayo imekwisha sajiliwa tayari kwa kuanza kazi pamoja na kusubiri utaratibu za kisheria ambazo zinatupasa kuwasilisha baadhi ya nyaraka hizo kwenye Tume ya Ushindani (FCC) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukamilisha taratibu kwa mujibu wa kisheria"

Alifafanua kuwa sheria ya FCC inawalazimu kusubiri siku120 ili kujiridhisha na utaratibu uliotumika ili timu hiyo ianze mfumo mpya wa uendeshaji.

"Mpaka sasa kampuni zote zote zimesajiliwa na sasa tunaelekea kwenye utaratibu wa mwisho ambao utatulazimu kusubiri kipindi hicho, taratibu za FCC zimeweka muda huo, lakini unaweza kupungua kutokana na wao kujiridhisha na maelezo kutoka kwetu maana hili ni jambo jipya na la kwanza kwa klabu kufanya mabadiliko ya uendeshaji

"Ukisikia klabu au taasisi imekamilisha mfumo wa uendeshaji lazima uipongeze kwani una taratibu nyingi za kufuatwa za kisheria mpaka kufanikisha, kwa sasa Simba ipo katika hatua ya mwisho na tunaamini tutafanikiwa," alisema Nghambi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’